MHE. CHANDE AKAGUA MIRADI MIPYA CHUO CHA UHASIBU (IAA)

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), akisikiliza maelezo kutoka kwa mhandisi wa majengo wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo hicho, jijini Arusha. Wa pili kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Cairo Mwaitete na watatu kushoto ni Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Mrisho Gambo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), akikagua ujenzi wa hosteli katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika chuo hicho, jijini Arusha. 

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa nne kulia), akikagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), wakati wa ziara yake fupi, jijini Arusha. Wa tatu kulia ni Naibu Mkuu wa Chuo cha IAA, anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Cairo Mwaitete na wapili kulia ni Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Mrisho Gambo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (wa nne kushoto), akimsikiliza Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), anayesimamia Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Cairo Mwaitete, wakati akimwelezea kuhusu kiwanda kidogo cha matofali yanayotumika katika ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo hicho, wakati wa ziara yake fupi, jijini Arusha. Wa tatu kushoto ni Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Mrisho Gambo.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Felician Mtahengerwa (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kushoto), Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Mipango, Fedha na Utawala, Dkt. Cairo Mwaitete (wa pili kulia), na Meneja wa Kampasi ya Arusha, Dkt. Grace Idinga (wa kwanza kulia), baada ya kukagua jengo la hosteli za Chuo hicho, wakati alipotembelea kukagua ujenzi wa miradi inayoendelea katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), jijini Arusha. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *