Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Oktoba 4, 2023 amekagua ukarabati unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa Ufunguzi wa Mashindano ya African Football League Oktoba 20, mwaka huu kati ya timu ya Simba na Al alhy ya nchini Misri.
Mhe. Kassim Majaliwa ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya Ukarabati huo kwa awamu ya kwanza, ambapo ameipongeza Timu ya Simba kwa kuweka baadhi ya vifaa katika Uwanja huo na kuwasihi wasiviondoe vifaa hivyo mara baada ya mchezo huo kumalizika ili viendelee kutumika katika uwanja huo.