Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kuzuia na Kukabiliana na Madhara ya El Nino Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango huo leo Oktoba 13, 2023 Jijini Dodoma.
Mpango huo umekabidhiwa kwa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wa baadhi ya Taasisi za Serikali