Na. Brown Jonas - WUSM
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekielekeza Chama cha Mchezo wa Magongo nchini (Baseball) kihakikishe kuwa mchezo huo unafika katika mikoa yote ya Tanzania Bara ili kupata vipaji zaidi katika mchezo huo.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo Desemba 8, 2023 Jijini Dar Es salaam alipokua akifungua mashindano ya Taifa ya mchezo huo katika uwanja wa shule ya Sekondari Azania
Dkt. Ndumbaro amesema ni muhimu kuanzisha vyama vya mchezo huo katika ngazi ya Mikoa na Wilaya ambavyo vitasaidia kuwaandaa vijana watakaowezesha kupatikana kwa ligi bora na timu ya Taifa
Pia amewaelekeza wahakikishe kuwa wanautambulisha mchezo huo kwenye shule mbwlimbali ili uweze kuingizwa katika mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA.
Na. Brown Jonas - WUSM
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa “BMT” kuhakikisha kuwa ifikapo Januari, 2024 kila klabu ya ligi kuu ya NBC iwe na Bima ya afya kwa wachezaji wake na iingizwe kwenye Kanuni ili kuwalinda wachezaji.
Mhe. Dkt. Ndumbaro amesema hayo Desemba 6, 2023 jijini Dar Es Salaam kwenye uzinduzi wa Taarifa ya Maendeleo ya Soko la Bima kwa Mwaka 2022.
"Kuanzia Januari mosi timu zote za Ligi Kuu zikate bima kwa wachezaji wote na hilo nikuagize Katibu Mtendaji wa BMT Neema Msitha hilo liingizwe kwenye kanuni tuwalinde wachezaji waweze kufanya vizuri,"amesema.
Aidha, Mhe. Ndumbaro amesema sekta ya michezo ina watu wengi sana hivyo ni muhimu kwa kampuni za bima kuangalia upande huo na kuwatumia kama sehemu ya kujitangaza.
Awali, Kamishna wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima “TIRA” Dkt. Baghayo Saqware amesema soko la Bima limekua kufikia trilioni 1.158 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.7
Ameshukuru Makampuni ya bima kwa kazi nzuri waliofanya ya kuongeza mapato na kulinda usalama wa mali na afya ya jamii.
Na Brown Jonas - WUSM
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan ambapo pamoja na mambo mengine viongozi hao wamejadili kuhusu tukio la mbio za pamoja za kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na India "The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman" linalotarajia kufanyika jijini Dar es salaam kati ya tarehe 30 na 31 Desemba,2023.
Akizungumza kuhusu tukio hilo leo Desemba 5, 2023 Mhe. Ndumbaro amesema Serikali ya India imeomba ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kufanikisha tukio hilo ambalo litahudhuriwa na mwanariadha maarufu kutoka nchini India Milind Soman.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi.Neema Msitha, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt.Kiagho Kilonzo na Makamu wa rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Wakili Evordy Kyando, Viongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Viongozi PAF Promotion Kampuni iliyoandaa pambano la Hassan Mwakinyo pamoja na Viongozi wa Mwakinyo Promotion akiwemo Bondia Hassan Mwakinyo mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Novemba 8 2023
Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao kati ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT), TPBRC, PAF na Mwakinyo Promotion kufuatia maelekezo ya Waziri kujadili na kufikia muafaka wa Mgogoro kati ya pande hizo.
Waziri amewataka wadau hao wa michezo kujadiliana na kupata hitimisho kwa manufaa ya pande zote na kwa maslahi ya Taifa.