WI-FI YA BURE YAZINDULIWA BENJAMIN MKAPA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye leo Novemba 5, 2023 Jijini Dar es Salaam amezindua huduma ya intaneti ya Wi-Fi katika Uwanja  wa Benjamin Mkapa ambayo itatumiwa na mashabiki wakati wa michezo mbalimbali itakayofanyika uwanjani hapo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuzinduliwa kwa huduma hiyo ni mwendelezo wa ukarabati unaofanyika katika katika uwanja huo.

Hafla hiyo pia imeshuhudiwa na Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Bw. Gerson Msigwa Naibu katibu Mkuu Bw. Nicholas Mkapa Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Mhandisi Peter Ulanga, huku  mashabiki pamoja na wapenda soka waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga nao wakishudia tukio hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *