Waziri Wa Maliasili Na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki Akimkabidhi Zawadi Mkurugenzi Wa Kimataifa Wa Mazingira, Maliasili Na Uchumi Wa Bluu Kutoka Benki Ya Dunia, Valerie Hickey Mara Baada Ya Kikao Cha Kujadili Kuhusu Utekelezaji Wa Mradi Wa Regrow Na Awamu Ya Pili, Pamoja Na Kushirikiana Katika Nyanja Nyingine Ikiwemo Biashara Ya Hewa Ya Kaboni Kwenye Misitu, Uchumi Wa Bluu Na Kuwajengea Uwezo Wanawake Katika Mnyororo Wa Thamani Wa Mazao Ya Nyuki. Kikao Hicho Kilichohudhuriwa Na Baadhi Ya Watendaji Kutoka Wizara Ya Maliasili Na Utalii Kimefanyika Leo Novemba 6, 2023 Jijini Dar Es Salaam.