MWIGULU NCHEMBA NDIO “MR CLEAN ” WA KIZAZI CHETU

Uongozi hupimwa kwa mambo mengi sana lakini kipimo cha juu zaidi kwa mujibu wa Carol S. Pearson, Mwandishi nguli wa masuala ya uongozi ni kipimo kitokanacho na uhalali wa kimaadili. Kwake yeye maadili ni nguzo mama katika kupima uwezo wa kiuogozi wa mtu yeyote katika utumishi wa umma.

Bunge lipo katika vikao vinavyojadili taarifa tatu muhimu za kiukaguzi. Kwanza taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC sambamaba na Kamatu tatu za Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa LAAC, PAC na PIC. Kitu kimoja kimevuta na kinavutia macho ya wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi na siasa na hiki ni moja wapo. HAKUNA MAHALA MWIGULU KATIKA TAARIFA ZOTE TATU ANATAJWA KUHUSIKA NA UPOTEVU WA HATA SENTI MOJA YA UMMA

Taarifa za CAG ni moja ya taarifa muhimu sana katika kutengeneza uhalali wa kimaadili katika utumishi wa umma wa ngazi ya juu kama uwaziri, na kwa vyovyote vile taarifa hii inapokupa uhalali au usafi humaanisha kwamba imekupa utakaso na usafi maana ndio kipimo cha juu kabisa cha ukaguzi na uwajibikaji katika fedha za umma. Hizi taarifa zote tatu za CAG kupita bila kumtaja popote si tu zinampa Mwigulu Nchemba positive impressions katika siasa zake lakini zaidi zinampa ubatizo halali wa kuitwa jina jipya la “Mr Clean”

Mwigulu anasifika kwa Uzalendo wake, kuwahurumia wanyonge na kusukuma maendeleo na kwa miaka yote hiyo ndio imekua sifa inayomtofautisha na wanasiasa wengi sana nchini. Kwa watu wenye kufuatilia masuala ya siasa, ni mara chache sana ripoti hizi zimekua zikipita bila kuwataja baadhi ya mawaziri kuhusika na upotevu au ubadhilifu wa fedha za umma, kikombe ambacho Mwigulu naona amekiepuka na kujipa uhalali wa kuitwa MR CLEAN.

SWALI kuu kwa sasa ni Je Mwigulu Nchemba ndio Mr Clean wa kizazi chetu kufuatia kupata uhalali wa usafi na taarifa zote za kikaguzi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *