WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO MHE. DKT. DAMAS NDUMBARO AKIZUNGUMZA NA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO NCHINI, WAKILI EVORDY KYANDO,

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Wakili Evordy Kyando, Viongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Viongozi PAF Promotion Kampuni iliyoandaa pambano la Hassan Mwakinyo pamoja na Viongozi wa Mwakinyo Promotion akiwemo Bondia Hassan Mwakinyo mara baada ya kikao cha pamoja kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, Novemba 8 2023

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao kati ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT), TPBRC, PAF na Mwakinyo Promotion kufuatia maelekezo ya Waziri kujadili na kufikia muafaka wa Mgogoro kati ya pande hizo.

Waziri amewataka wadau hao wa michezo kujadiliana na kupata hitimisho kwa manufaa ya pande zote na kwa maslahi ya Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *