MHE. MWINJUMA AIAGIZA BMT KUTATUA CHANGAMOTO ZA AAT

Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lihakikishe kuwa linakutana na Chama cha Mbio za Magari nchini (AAT) ili kuangalia namna ya kukisaidia Chama hicho kipate hekari 20 kilizoomba kwa ajili ya eneo la mashindano na mafunzo.

Mhe. Mwinjuma ametoa kauli hiyo wakati akihitimisha Mashindano ya mbio za magari ya Afrika (African Rally Championship) Novemba 12, 2023 katika Shamba la Miti SaoHill wilayani Mufindi, yaliyoanzia katika Shamba la ASAS Mkoani Iringa Novemba 11, 2023.

Amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imepewa jukumu la kusimamia michezo yote nchini ili iwe na ufanisi mkubwa kwa kuwa michezo ni ajira kutokana na mchango wake katika mapato ya nchi.

” Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatutaka kusimamia michezo yote nchini, hivyo tumeendelea kuhudumia maono hayo katika kuhakikisha tunasimamia michezo yote ili ilete tija kwa Taifa.” Amesisitiza Mhe. Mwinjuma

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya ASAS, yamefanyika pamoja na Mashindano ya magari ya Taifa (National Rally Championship ) yanatarajiwa kufanyika tena kwa mara ya pili mfululizo mwaka 2024 mkoani Iringa, huku Kampuni hiyo ikiahidi kuendelea kudhamini mashindao hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *