SERIKALI INAKUSANYA WASTANI WA TRILIONI 2 KWA MWEZI KATIKA MWAKA WA FEDHA.

Serikali inakusanya wastani wa trilioni mbili kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2022/23 ikilinganishwa na mwaka 2021/22 ambapo makusanyo yalifikia shilingi trilioni 1.86 kwa mwezi ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 8.2. Aidha, mwezi December 2022, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanikiwa kukusanya shilingi trilioni 2. 79, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya makusanyo yote ya mwezi tangu Tanzania ipate uhuru.

Mhe. Chande aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mafanikio haya na pia kwa mageuzi makubwa ambayo Mamlaka imeyajenga katika taswira nzima ya kazi ya ukusanyaji kodi.Serikali inakusanya wastani wa trilioni mbili kwa mwezi katika mwaka wa fedha 2022/23 ikilinganishwa na mwaka 2021/22 ambapo makusanyo yalifikia shilingi trilioni 1.86 kwa mwezi ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 8.2. Aidha, mwezi December 2022, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanikiwa kukusanya shilingi trilioni 2. 79, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi ya makusanyo yote ya mwezi tangu Tanzania ipate uhuru.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlipa Kodi yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

“Wastani wa makusanyo kwa mwezi mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2022/23 yalikuwa ni shilingi trilioni 2 wakati makusanyo kwa mwaka mzima yalikuwa trilioni 24 ikilinganishwa na mwaka 2021/22 iliyokuwa na makusanyo kwa mwezi wastani wa shilingi trilioni 1.86 na makusanyo kwa mwaka mzima yalikuwa trilioni 22.28,” Alisema Mhe. Chande.

Alisema ufanisi umeimarika kwani wastani wa makusanyo kwa mwezi katika mwaka wa kwanza wa shughuli za Mamlaka mwaka 1996 yalikuwa bilioni 42.

Hata hivyo alisema TRA ilichukua hatua za kimkakati Zanzibar ili kuongeza ufanisi jambo ambalo walifanikiwa. “Makusanyo ya mapato kutoka Zanzibar ambayo yaliyokuwa yakilegalega katika kipindi kirefu cha nyuma, sasa yameimarika,” Aliongeza Mhe. Chande.

Mhe. Chande aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa mafanikio haya na pia kwa mageuzi makubwa ambayo Mamlaka imeyajenga katika taswira nzima ya kazi ya ukusanyaji kodi.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mlipa Kodi yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yaliyofanyika jana usiku katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.

Wastani wa makusanyo kwa mwezi mpaka mwisho wa mwaka wa fedha 2022/23 yalikuwa ni shilingi trilioni 2 wakati makusanyo kwa mwaka mzima yalikuwa trilioni 24 ikilinganishwa na mwaka 2021/22 iliyokuwa na makusanyo kwa mwezi wastani wa shilingi trilioni 1.86 na makusanyo kwa mwaka mzima yalikuwa trilioni 22.28,” Alisema Mhe. Chande.

Alisema ufanisi umeimarika kwani wastani wa makusanyo kwa mwezi katika mwaka wa kwanza wa shughuli za Mamlaka mwaka 1996 yalikuwa bilioni 42.

Hata hivyo alisema TRA ilichukua hatua za kimkakati Zanzibar ili kuongeza ufanisi jambo ambalo walifanikiwa. “Makusanyo ya mapato kutoka Zanzibar ambayo yaliyokuwa yakilegalega katika kipindi kirefu cha nyuma, sasa yameimarika,” Aliongeza Mhe. Chande.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *