Na Brown Jonas
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna.
Katika kikao hicho kilichofanyika Novemba 25, 2023 Jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine wamejadili juu ya ushirikiano wa kuendeleza sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuibua na kukuza vipaji hapa nchini.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Gerson Msigwa, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Bw. Abel Shirima, Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Ally Mayay Tembele, Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Deogratius Mbinga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha Pamoja na watendaji wengine wa Benki hiyo.