Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amefungua Mkutano wa Pamoja wa Wenyeviti wa Bodi ya Wakurugenzi na Washirika wa Maendeleo wa TradeMark Afrika (TMA), Leo tarehe 28 Novermba,2023, katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo, Wajumbe hao wamejadili kwa pamoja fursa na changamoto za utekelezaji wa Miradi inayofadhiliwa na TradeMark Afrika, ambayo inalenga kuwezesha na kuimarisha biashara katika nchi wanachama.
Aidha, wajumbe wamejadili namna ya utekelezaji wa Miradi hiyo na namna ya kuimarisha Miundombinu, Mifumo, Sheria za Biashara na Uwekezaji, hususan katika kipindi hiki cha utekelezaji wa Soko Huru la Afrika (AFCFTA)