Bodi ya Utalii Tanzania, Ofisi ya kanda ya Kusini kwa kushirikiana na wadau wa Utalii imeanza kampeni yake maalumu ya kuhamasisha utalii wa ndani iliyopewa jina la ROYAL TOUR CHRISTMAS MBUGANI.
Akizungumza na Nuru FM Afisa kutoka Bodi ya Utalii Kanda ya Iringa Hozza Mbura amesema kuwa Kampeni hiyo ina lengo la kuhamasisha utalii wa ndani hususani katika msimu huu wa sherehe za siku kuu ya CHRISTMAS.
Amesema kuwa Kampeni hiyo inaratibiwa Bodi ya Utalii ofisi ya kanda ya kusini kwa kushirikiana na kampuni ya Utalii ya Bateleur tour and Safaris, @bateleur_safaris_and_tours_ltd kampuni ya Mkuta travel na Kampuni ya UPL SAFARIS ambazo zimeandaa vifurushi maalumu vya utalii ( Tour packages) katika sehemu mbalimbali za vivutio vya utalii Ikiwemo Hifadhi ya Taifa Ruaha, @ruaha_national_park Hifadhi ya milima ya Udzungwa, @udzungwamontain_national_park Mpanga kipengere @mpangakipengeregame pamoja na maeneo ya kihistoria ya kalenga/Mkwawa Museum na ISIMILA stone age site.
“Kampeni hii ni mahususi haswa katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii, tunataka tuone watanzania na wanakusini kwa ujumla wanajitokeza kwa wingi katika kampeni hii maalumu na wanatembelea vivutio vya utalii vya kusini katika msimu huu wa likizo na sherehe za Christmas pamoja na mwaka mpya. Na hii ni kuunga mkono jitihada za alizozoanzisha Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kampeni yake ya Tanzania The Royal tour”
Mbura amebainisha kuwa matarajio yao kama Bodi kuona wanachi wanajitokeza kwa wingi na kufurahia kwa pamoja katika moja ya vivutio vinavyopatikana kusini mwa Tanzania.
Amesema kwa wale ambao watataka kufanya nao Kampeni hiyo wanatakiwa kuwasiliana na Ofisi ya Bodi ya Utalii ofisi ya Kanda kusini kupitia namba za simu 0715088871 au kupitia Ukurasa wao wa mitandao ya kijamii