
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo,Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa wito kwa wadau wa Bima yakiwemo Mashirika yanayotoa huduma za bima na taasisi za kifedha ziongeze ushiriki katika kukuza maendeleo ya michezo hapa nchini.

Akizungumza leo, Desemba 02, 2023, wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Exim Bima Festival, Mhe. Mwinjuma ameyaomba makampuni hayo yajitoe zaidi katika kuwekeza katika timu za michezo kama vile Ligi Kuu na Ligi daraja la kwanza kwa kuwa uwekezaji huo utayawezesha kujitangaza zaidi.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya mashirikia kuwekeza kwenye sekta za michezo itachangia maendeleo na ustawi wa michezo nchini na kuimarisha uhusiano kati ya sekta ya bima na michezo kwa manufaa ya pande zote.
