Mcheza Tennis mashuhuri duniani, John McEnroe, ameshinda kwa mara ya kwanza mchezo maalum wa Tennis Serengeti baada ya kumpiku mchezaji mwingine nguli ambaye ni mdogo wake Bw. Patrick McEnroe.
Mchezo huo umechezwa leo katikati ya Hifadhi ya Serengeti na kuweka historia ya aina yake duniani kuwa mechi ya kwanza kuchezwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa mchezo huo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vikombe, Patrick, kwa niaba ya kaka yake na wenzao waliokuja Tanzania wameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuomboleza na kutoa pole kwa waathirika wote wa mafutiko yaliyotokea mjini Katesh, Hanang.