Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi na Takwimu Bw.Daniel Msolwa akipongeza COSOTA kwa kufanya utafiti wa kuhuisha taarifa za utafiti wa mchango wa pato la taifa katika Hakimiliki uliofanywa na Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) kwa kushirikiana na COSOTA na BRELA zilizotangazwa mwaka 2012 katika kikao kilichofanyika Disemba 05,2023 Jijini Dodoma baina ya COSOTA na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare akizungumza umuhimu wa kuhuwisha utafiti wa mchango wa Hakimiliki katika Pato la Taifa uliofanyika 2009-2010 kwa ufadhili wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) katika kikao chake na Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt.Albina Chuwa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kilichofanyika Disemba 05,2023 Jijini Dodoma.
Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt.Albina Chuwa akizungumzia mchango wa Ofisi yake katika kufanikisha utekelezaji wa utafiti wa kubaini namna hakimiliki inachangia pato la Taifa, Disemba 05,2023 Jijini Dodoma katika kikao na COSOTA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Doreen Anthony Sinare pamoja na Maafisa wa COSOTA.