WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS FEDHA NA MIPANGO, MHE. DKT. SAADA SALUM MKUYA (MB), AKIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI MWANDAMIZI WA BENKI YA DUNIA, BW. AXEL VAN TROTSENBURG WALIPOTEMBELEA MIRADI YA UFUGAJI SAMAKI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya (Mb), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bw. Axel van Trotsenburg , walipotembelea miradi ya ufugaji samaki na udhibiti wa maji ya Bahari ya Hindi kuingia kwenye mashamba na maeneo ya makazi ya watu, unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), katika kijiji cha Bumbwini-Mafufuni,

Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini, Zanzibar, ambao umewezeshwa na Benki ya Dunia kupitia Mfuko wa IDA.

Benki ya Dunia, itawezesha zaidi ya dola za Marekani milioni 883, na tayari imetoa zaidi ya dola 650 zimetolewa kwa ajili ya kusaidia Kaya Masikini Visiwani Zanzibar, ambapo katika eneo hilo la Bumbwini, wananchi 467 wamenufaika wakiwemo wengine 280 waliowezeshwa fedha za kuwekeza kwenye miradi midogomidogo inayowasaidia kujikimu kimaisha.

Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bw. Axel van Trotsenburg , akipata maelezo juu ya mradi huo wa ufugaji samaki pindi walipotembelea miradi ya ufugaji samaki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya (Mb), akiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bw. Axel van Trotsenburg, na wajumbe wengine waliombatana nao walipotembelea miradi ya ufugaji samaki

Mkurugenzi Mtendaji Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Bw. Axel van Trotsenburg , akiwa katika miradi ya ufugaji samaki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *