Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, ametoa wito kwa viongozi wa vyama vinavyojihusisha na Sanaa na Utamaduni kushiriki kozi fupi zinazotolewa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) akibainisha kuwa kuwepo kwa viongozi hao kwenye tasnia ya sanaa kwa muda mrefu pekee hakutoshi kuwawezesha kuwa viongozi bora kwa kuwa kozi hizo zitawasaidia kuwa viongozi wanaoelewa kikamilifu wajibu wao.
Mhe. Mwinjuma alitoa kauli hiyo Desemba 8, 2023, wakati wa mahafali ya 34 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo ambapo alikabidhi vyeti kwa wahitimu 270, Kati yao, Astashahada wakiwa 158 (Wanaume 119 na Wanawake 39), na Stashahada wahitimu 112 (Wanaume 86 na Wanawake 26).
Kuna uwezekano tukabadilisha mpaka kanuni kwamba mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi kwenye vyama na mashirikisho ya Sanaa na Utamaduni inabidi awe na cheti cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.Kimsingi kushiriki kwenye shughuli za Sanaa muda mrefu hakukupi uwezo wa kiungozi, unapata maarifa na uelewa ya kipi kinachofanyika kwenye Sanaa lakini pengine unakosa uwezo wa uongozi wa kipi kinatakiwa kufanyika ili kuongoza hao ambao umewaomba nafasi ya kuwaongoza” Amesisitiza Mhe. Mwinjuma.
Katika mahafali hayo Naibu Waziri Hamis Mwinjuma aliwakabidhi vyeti vya kuhitimu mafunzo ya kozi fupi ya Uongozi, Biashara na Utawala katika Sanaa washiriki 16 waliofuzu mafunzo hayo wakiwemo wasanii na baadhi yao ni viongozi wa mashirikisho na vyama vya sanaa hapa nchini Tanzania, akiwemo Farid Kubanda, maarufu kama Fid Q.

Naibu Waziri wa wizaraya Utamaduni sanaa na michezo Hamis Mwinjuma
Wahitimu