RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIBONYEZA KITUFE KUASHIRIA UZINDUZI WA MCHAKATO WA UKUSANYAJI MAONI KUTOKA KWA WANANCHI KUHUSU DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria uzinduzi wa Mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 09 Desemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete kushiriki Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili katika viwanja vya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara 09 Desemba, 2023

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *