Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe. Samia suluhu hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua mchakato wa ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kuhusu dira ya taifa ya maendeleo 2050
Rais Samia alifanya uzinduzi huo wakati wa Maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.