Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, Bw. Robert Manyama, akitoa hotuba wakati wa Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania – TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dare es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uelewewa Wahariri hao kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha kuhusu majukumu ya Taasisi hiyo inayolenda kusuluhisha malalamiko ya kikodi baina ya wadau na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Meneja wa Malalamiko na Usajili kutoka Taasisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, Bi. Naomi Mwaipola, akizungumza jambo wakati wa Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania -TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo wahariri hao kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia hotuba iliyokua inatolewa na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, Bw. Robert Manyama (hayupo pichani), wakati wa Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania – TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Mawasiliano kwa Umma kutoka Taasisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, Bw. Edwin Iwato, akizungumza wakati Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania – TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dare es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja, akielezea Mkakati wa Mawasiliano wa Wizara kuhusu namna ilivyojipanga na kuendelea kuwashirikisha Wahariri na Vyombo vya Habari kwa ujumla ili kuwajengea uelewa wadau wa ndani na nje ya nchi wa Wizara ya Fedha wakati wa Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania; TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia hotuba iliyokua inatolewa na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania, Bw. Robert Manyama (hayupo pichani), wakati wa Kikao Kazi cha Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania – TOST) iliyopo chini ya Wizara ya Fedha na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dare es Salaam. Kikao hicho kimelenga kuwajengea uwezo kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania kutoka Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania; TOST), Bw. Robert Manyama (wapili kulia walioketi), Meneja wa Malalamiko na Usajili kutoka Taasisi hiyo, Bi. Naomi Mwaipola (wa pili kushoto walioketi), Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Mawasiliano kwa Umma kutoka Taasisi hiyo, Bw. Edwin Iwato (wa kwanza kulia walioketi) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (wa kwanza kushoto walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha Taasisi hiyo na Wahariri hao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, ambapo Kikao hicho kililenga kuwajengea uwezo Wahariri hao kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Tanzania kutoka Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ((Tax Ombudsman Service of Tanzania – TOST), Bw. Robert Manyama (Katikati), Meneja wa Malalamiko na Usajili kutoka Taasisi hiyo, Bi. Naomi Mwaipola (wa pili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Elimu na Mawasiliano kwa Umma kutoka Taasisi hiyo, Bw. Edwin Iwato (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini, baada ya kumalizika kwa kikao kazi cha Taasisi hiyo na Wahariri hao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dare es Salaam, ambapo Kikao hicho kililenga kuwajengea uwezo Wahariri hao kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo ili wawe na uwezo wa kuwahabarisha wananchi kwa ufasaha.
Na. Scola Malinga na Saidina Msangi, WF, Dar Es Salaam.
Ofisi ya Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST), imekaribisha wananchi wenye changamoto zinazohusiana na kodi kuwasilisha malalamiko katika Taasisi hiyo ili ziweze kushughulikiwa ndani ya siku 30.
Wito huo imetolewa na Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi Bw. Robert Manyama, alipokutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Hazina Ndogo, alipokuwa akiitambulisha Ofisi hiyo pamoja na malengo na wajukumu ya kuundwa kwa Taasisi hiyo huru ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (Tax Ombudsman Service of Tanzania TOST).
Bw. Robert Manyama alisema kuwa Taasisi hiyo imeanzishwa kama jukwaa huru la kutoa usuluhishi wa malalamiko na taarifa za kodi kwa kuzingatia haki na usawa kwa mlalamikaji na mlalamikiwa.
Alisema kuwa Taasisi hiyo imeundwa na Serikali ikiwa na lengo la kushughulikia malalamiko ya walipa kodi yanayotokana na taratibu huduma na maamuzi ya kiutawala, yanayotokea wakati wa usimamizi wa sheria za kodi unaofanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
‘‘Taasisi ya TOST jukumu la kuainisha maeneo yenye matatizo katika usimamizi wa sheria za kodi na ambayo ni vyanzo vya malalamiko ya walipa kodi nchini na kutoa mapendekezo ya marekebisho kwa Waziri wa Fedha, alifafanua Bw. Manyama.
Alieleza kuwa TOST inalenga kupunguza mlundikano wa kesi mahakamani na kuwezesha upatikanaji wa suluhu kwa haraka na kwa usawa dhidi ya malalamiko yatokanayo na usimamizi wa sheria za kodi.
Bw. Manyama alisema TOST pia ina lengo la kuongeza imani ya wananchi dhidi ya mfumo wa usimamizi na ukusanyaji kodi nchini na ulipaji wa kodi kwa hiari kwa kuhakikisha kwamba taratibu na huduma sitahiki za usimamizi wa kodi zinafuatwa bila unyanyasaji.
‘‘Mtu yeyote ambaye haridhishwi na utendaji katika maeneo hayo niliyotaja ya utoaji wa huduma, taratibu na maamuzi za Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), anaweza kuwasilisha lalamiko kwa Msuluhishi ndani ya siku 90 tangu kutokea ili liweze kufanyiwa kazi, usuluhishi wa malalamiko ya kodi kwa wakati utapunguza kwa kiasi kikubwa pingamizi za kodi na migogoro ambayo isiyo na ulazima wa kupelekwa mahakamani’’, alifafanua Bw. Manyama.
Alisema kwa mujibu wa sheria malalamiko ya mlipakodi yanayakiwa kushughulikiwa ndani ya siku 30 na kuwasilisha taarifa kwa Waziri wa Fedha ndani ya siku 14, hivyo amehimiza walipakodi kutoa taarifa zinazohitajika kwa haraka zinapohitajika ili kuepuka kuchelewesha mchakato wa kushughulikia malalamiko yao.
Aliongeza kuwa dhamira ya Taasisi hiyo ni kushughulikia malalamiko ya kodi kwa usawa na kwa ufanisi, kutatua malalamiko dhidi ya usimamizi wa sheria za kodi kwa njia ya majadiliano na upatanishi huku ikiharakisha utatuzi wa malalamiko kwa kutumia taratibu zisizo na gharama kubwa au kuhitaji mwanasheria jambo litakalojenga imani ya walipa kodi kwa mfumo wa usimamizi na ukusanyaji wa kodi nchini.
Naye Meneja wa Malalamiko na Usajili Bi. Naomi Mwaipola, alisema kuwa Taasisi hiyo inatoa huduma bure kwa wananchi na imejipanga kuwahudumia wananchi katika mikoa yote nchini na kutoa rai kwa wahariri hao kufikisha taarifa kwa umma.
‘‘Ninatazamia na ninawaamini kuwa ninyi ni wajumbe wazuri kwa haya mliyosikia na mtapeleka ujumbe kwa Watanzania watakaokuwa wanahitaji huduma yetu na tunafika popote licha ya kuwa Makao Makuu yetu yapo Dodoma, ukiwa mkoa wowote unaruhusiwa kuleta changamoto yako na sisi tutakufikia,’’akisema Bi. Mwaipola.
Taasisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) ilianzishwa mwaka 2019 kwa marekebisho yaliyofanywa katika sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 na inafanya kazi nchi nzima, na mifumo yake imeanza kujengwa mwaka 2023 ambapo imeanza rasmi kutoa huduma kwa wananchi.
MWISHO.