Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizindua Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za kibenki za Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akibadili namba ya siri ya kadi yake mpya ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), baada ya ya kuzindua Tawi la Benki hiyo jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb), akizungumza na wananchi baada ya kuzindua Tawi la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb), akionesha zawadi ya saa aliyokabidhiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), baada ya kuzindua Tawi la Benki hiyo, jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Dkt. Muhsin Salim Masoud.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb), akionesha zawadi ya saa aliyokabidhiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), baada ya kuzindua Tawi la Benki hiyo, jijini Dodoma, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ, Dkt. Muhsin Salim Masoud.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Dkt. Muhsin Salim Masoud, wakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Rosemary Senyamule, baada ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) akiagana na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Mhe. Ali Suleman Ameir, baada ya hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF – Dodoma)
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka watanzania kutumia benki kuhifadhi fedha zao ili kuhakikisha usalama wa fedha zao na usalama wao na kuacha tabia ya kuhifadhi fedha majumbani.
Dkt. Nchemba aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akizundua Tawi la Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo na kushindwa kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa.
Dkt. Nchemba alisema ni vema wananchi wakajenga utamaduni wa kutumia benki kwa kuwa uendeshaji wa uchumi wa kisasa unategemea zaidi matuminzi ya utaratibu wa kibenki ambao kwa sasa umerahisishwa na unapatikana kwa urahisi.
“Utaratibu wa kuchimbia fedha ni utataribu wa kizamani, benki sasa zipo kiganjani kwanini uchimbie fedha? Popote ulipo unawezakupata huduma za benki”, alisisitiza Mhe. Nchemba.
Dkt. Nchemba alisema Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na benki zote hapa nchini kama utekelezaji wa sera jumuishi za masuala ya kifedha na kiuchumi zinazolenga kuwasogezea wananchi huduma karibu hasa hizi za kifedha.
‘’Naomba kutumia fursa hii kuwaomba wafanyabiashara, watumishi wa umma na binafsi, viongozi wa Serikali wa ngazi mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuiunga mkono na kuitumia Benki ya PBZ katika shughuli zetu za kiuchumi, kwani benki hii imekuwa ikitoa huduma zake kwa uaminifu mkubwa na kwa riba nafuu.’’
Akitoa salamu za Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Zanznibar, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Ali Suleiman Amir alisema Serikali imeamua kuhakikisha huduma za fedha zinawafikia wananchi wote kwa urahisi.
Aliipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kutimiza azma ya Serikali kwa kufungua matawi yao katika maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Mtendaji wa PBZ, Dkt. Muhsin Salim Masoud, alisema kuwa Benki hiyo ina vituo vya kutolea huduma takribani 45 ambapo vituo 34 vipo Zanzibar na vituo 11 vikiwa Tanzania Bara huku akiahidi kuongeza vituo vya kutolea huduma ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.
‘’Katika mpango kazi wetu, mwakani tutafungua kituo katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Mwanza, Arusha na Tanga ili kuwafikia Watanzania wengi na kuwapatia huduma za kifedha kwa gharama nafuu sana’’, alibainisha Dkt. Masoud.
Aliongeza kuwa Benki hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kupata tuzo ya mlipaji kodi bora Zanzibar iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuongezeka kwa faida, kufuatia juhudi mbalimbali zilizofanywa kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa weledi.
‘’Mafaniko ya Benki hii yametokana na Sera nzuri za Fedha hapa Nchini, Sera nzuri za Benki ya PBZ, mahusiano mazuri ya wateja, huduma zenye gharama nafuu na juhudi za wafanyakazi wa Benki yetu’’, alisema Dkt. Masoud.
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ni Taasisi ya kifedha inayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa asilimia mia moja. Benki hiyo ilianzishwa mwaka 1966 kwa lengo la kutoa huduma za kifedha kwa wananchi ambapo kwa sasa inamtaji wa takribani bilioni 150.
Mwisho.