HAYATI NYERERE KUPEWA TUZO YA KISWAHILI DUNIANI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali itazindua Tuzo ya Kimataifa ya Kiswahili kwa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere ili kuenzi mchango wake katika kukuza Kiswahili duniani

Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo Desemba 15, 2023 wakati wa kongamano la 8 la Kiswahili lililoandaliwa na Chama Cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) Jijini Arusha.

Mhe. Ndumbaro amesema tuzo hizo zitatolewa katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa ikiwa ni heshima ya Shirika hilo kuitambua lugha ya Kiswahili duniani na kutenga Julai 7 kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.

Ameongeza kuwa katika tuzo pia watu wengine waliojitoa kukuza Kiswahili watatambuliwa na kupewa tuzo kwa heshima ya Baba wa Taifa

Kongamano hilo limehudhuriwa na washiriki kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Ufaransa, Marekani, Malawi, Kenya na Uganda ambapo mijadala mbalimbali ya kubidhaisha Kiswahili imejadiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *