RAIS DK. MWINYI AKUMBUSHA UMUHIMU WA AMANI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na baadae kushiriki Dua Maalum ya kumuombea iliyoandaliwa na Jumuiya ya Fysabilillah Tabligh Markaz Zanzibar Msikiti wa Mwembe Shauri, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 15 Desemba 2023.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema siasa zimetulia, amani ipo, watu ni wamoja tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aidumishe amani iliyopo , umoja na mshikamano kwa watu na upendo.

Pia ameushukuru Uongozi wa ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar kwa uratibu mzuri wa shughuli za dini nchini

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali , Chama cha Mapinduzi na Dini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *