
Viongozi wa Dini wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.


Viongozi wa Dini wakiwa kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Ofisi za Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha usalama wa nchi na mipaka yake dhidi ya majanga mbalimbali unaendelea kuimarishwa ili kujiandaa na kuwa na utayari wa kukabiliana na majanga, maafa na dharura yoyote.
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Machi 14, 2024) wakati wa ufungaji wa mafuzo ya zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi Tanzania, katika viwanja vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Bandarini jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa moja ya jitihada hizo ni pamoja na kukamilisha maandalizi ya nyaraka mbili muhimu za Mpango wa Kitaifa wa Maafa ya Kikemikali, Kibaiolojia, Kiradiolojia na Kinyukilia. (CBRN National Action Plan) na Mpango wa Kuitikia wakati wa Dharura za Kinyuklia na Kiradiolojia (Radiological and Nuclear Response Plan) ambazo alizizindua katika hafla hiyo.
“Kupitia nyaraka hizi, mmeweka mikakati ya pamoja ya kitaifa ya namna ya kukabiliana na kujikinga na majanga yatokanayo dharura za kikemikali, kibaiolojia, kiradiolojia na kinyuklia. Nimefurahi sana kusikia nyaraka hizo zimezingatia masuala muhimu ya kisera, uzoefu wa kukabiliana na majanga kitaifa na kimataifa pamoja na matakwa ya kisheria na itifaki za kimataifa.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka wizara zote na taasisi zinazohusika na kutekeleza mipango hiyo kuitumia kikamilifu na zitoe ushirikiano kwa wote wanaohitaji kutekeleza miongozo hiyo “Miongozo hii isiwe ni nyaraka za makabatini tu bali iwe miongozo ya utekelezaji wa hatua thabiti za kuhakikisha tunajenga nchi imara na salama. ”
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mafuzo ya zoezi la utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi yalilenga kuwapa washiriki maarifa na ujuzi wa kukabiliana na vitisho vya kikemikali, kiradiolojia, kinyuklia na kusaidia juhudi kujiandaa na kukabiliana na majanga hayo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongeza kuwa nyaraka zilizozinduliwa na Mhe. Majaliwa zitatumika kuwa nyaraka za kitaifa na miongozo inayochukua mitizamo na mahitaji ya taasisi na wizara mbalimbali za Serikali na wadau wengine waliopewa majukumu katika nyanda za kemikali, kibaolojia, kiradiolojia na nyuklia “Lengo kuu la mipango hii ni kuweka mikakati ya pamoja kama Taifa ya namna ya kukabiliana na kujikinga na majanga hayo. ”
Kwa Upande wake, Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko amesema kuwa mazoezi ya utayari dhidi ya dharura za kikemikali na kimionzi yataendelea kufanyika mara kwa mara kwa lengo la kujenga utayari wa timu ya Taifa ya kujiandaa kukabiliana na dharura za kitaifa.
Wizara ya Fedha kupitia Shirika la Kijamii linalojishughulisha na utoaji Elimu ya Uraia (TACCI) wamefanikiwa kuwafikishia elimu ya Fedha baadhi ya wakazi wa Morogoro kwa njia ya Sanaa ikiwa ni mwanzo wa mkakati wa kufikisha elimu hiyo nchi zima ili kutekeleza Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa kwaka 2021/2022 hadi 2029/2030.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi wa Chapa na Uchapishaji kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Edward Haule kuhusu shughuli mbalimbali za uchapaji wa Mitihani pamoja na Nyaraka mbalimbali wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza hilo Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kibao cha Uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwenye hafla iliyofanyika katika Ofisi za Baraza hilo Kijitonyama - Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Watoto wa Shule ya Msingi Kisutu wakati wakitumbuiza mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2023.