DKT. NCHEMBA AWATAKA WAFANYABIASHARA NCHINI KULIPA KODI KWA UAMINIFU

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba Madelu (Mb), amesema kuwa wakati Serikali inafanya kila jitihada kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini,

wafanyabiashara kwa upande wao wanatakiwa kulipakodi stahiki pamoja na baadhi yao kuacha kukwepa kodi, ikiwemo kutotoa risiti, kutoa risiti zisizolingana na thamani halisi ya bidhaa au huduma iliyotolewa, vitendo ambavyo alisema vinaikosesha Serikali mapato hivyo kukwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa wito huo wakati akizungumza katika Mkutano wa Wawekezaji wa Ndani, ulioandaliwa na Wizara ya Kilimo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam

Mawaziri walioshiriki mkutano huo, waziri Hussein Bashe, Kitila Mkumbo, Mwigulu Nchema na mkurugrnzi mkuu wa crdb bank

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *