WAZIRI WA MADINI MHE. ANTHONY PETER MAVUNDE AMEWATAKA WAMILIKI LESENI ZA MADINI NCHINI KUZIENDELEZA LESENI

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Peter Mavunde amewataka wamiliki Leseni za Madini nchini kuziendeleza leseni husika kwa mujibu wa Sheria inavyoelekeza kwa kuwa zipo leseni nyingi ambazo hazifanyiwi kazi na hivyo kuzorotesha ukuaji wa kasi wa Sekta ya Madini.

Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Wilayani Ruangwa, Mkoa wa Lindi wakati alipotembelea Mgodi wa Madini Kinywe wa Lindi Jumbo ambao unatarajia kuanza uzalishaji mwishoni mwa mwezi Machi, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *