WAZIRI WA FEDHA, MHE. DKT. MWIGULU NCHEMBA (MB), AMESHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO KWA KUSHIRIKI IBADA

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kushiriki Ibada na Waumini wa Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheti Tanzania (KKKT)-Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Usharika wa Kimara huku akiwasihi Watanzania kumuombea Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na nchi kwa jumla.

Katika salamu zake kwa niaba ya Serikali, Mhe. Dkt. Nchemba, alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha nishati ya umeme kupitia Gridi ya Taifa na tayari imeiunganisha katika gridi ya Taifa mikoa ambayo ilikuwa haijafikiwa na umeme, lakini pia imeendelea kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kufua Umeme la Mwl. Julius Nyerere ambapo Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilipokea mradi ukiwa chini ya asilimia 37 na hivi sasa mradi umefikia zaidi ya asilimia 94 na litaanza kuzalisha umeme hivi karibuni.

Wakati huohuo, Mhe. Dkt Nchemba alisema kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi ameendelea kuboresha mazingira kwa wawekezaji wa viwanda, sekta za elimu, afya, maji na miradi mingine mbalimbali kwa kuboresha mazingira yake tofauti na alivyoipokea nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *