Related News
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (IMO), Bw. Arsenio DomÃnguez, jijini London.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb) amekutana na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo na Mabadiliko ya Tabianchi wa Denmark, Mhe. Dan Jørgensen ambapo nchi hizi mbili zimeangazia maeneo ya ushirikiano na kukubaliana kuongeza ushirikiano kwenye sekta za kimaendeleo.
Tanzania na Denmark zinaenda kuongeza ushirikiano kwenye maeneo ya biashara, miundombinu, umeme, uwekezaji, kubadilishana uzoefu kwenye teknolojia pamoja na nishati safi na salama ikiwa ni sehemu ya kutunza mazingira na tabianchi kwa manufaa ya jamii ya sasa na baadaye.
Pande zote mbili zimeonesha kufurahishwa na mwelekeo wa ushirikiano huu ambapo Denmark ilionesha dhamira hiyo kwa vitendo mwaka 2023 baada kutengua uamuzi wake wa kuufunga ubalozi wake nchini.
Waziri Jørgensen yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili inayotarajiwa kufikia tamati hapo kesho.
DKT. SALIM AHMED SALIM
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Msahariki January Makamba Leo amepata fursa ya kumtembelea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Hussein mwinyi kutoa mkono wa pole kwa msiba wa Mzee Ali Hassan Mwinyi na kumpa maelezo ya utendaji wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar.
Ushawishi wa Tanzania Duniani utategemea na Ubora wa Sera ya Mambo ya Nje inayorekebishwa .
Imeelezwa kuwa ili Tanzania iweze kufikia malengo ya Maendeleo iliyojiwekea, lazima iwe na Sera Bora ya Mambo ya Nje inayozingatia maoni na matakwa ya makundi yote ya wadau nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Mhe. Ali Suleiman Ameir ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano la wadau la kukusanya maoni kuhusu marekebisho ya Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 lililofanyika kwenye Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 05 Februari 2024.
Kongamano hilo ambalo ni la tatu kufanyika ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kushirikisha wananchi kutoa maoni yatakayozingatiwa katika zoezi la kurekebisha Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.
Mwenye dhamana ya kusimamia Sera hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba ametaja sababu za Wizara yake kuratibu makongamano hayo ambapo alisema linalofuata litafanyika Pemba tarehe 10 Februari 2024.
Alieleza kufanyika kwa makongamano hayo ni utekelezaji wa misingi ya utawala bora ambayo inasisitiza umuhimu wa kushirikisha wadau katika utungaji wa Sera za nchi, ikiwemo Sera ya Mambo ya Nje.
Alieleza pia kuwa Sera ni Tamko linalotoa mwongozo namna nchi itakavyoshughulikia ushirikiano na uhusiano wake na dunia. Hivyo, utungaji wa Tamko muhimu kama hilo lazima lishirikishe wadau wote.
Mhe. Makamba aliwambia washiriki wa Kongamano hilo kuwa Tanzania ina ushawishi mkubwa duniani tofauti na nguvu zake za kiuchumi na kijeshi kutokana na kuwa na Sera bora ya Mambo ya Nje. Hivyo, ili iendelee kuwa na ushawishi huo duniani lazima itungwe Sera imara itakayozingatia maoni ya wadau wote.
Aliendelea kueleza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ina uhusiano wa moja kwa moja na malengo ya Maendeleo ya nchi. Hivyo, mchakato wa utungaji wa Sera ya Mambo ya Nje lazima ushirikishe wadau kwa kuwa maendeleo ni jambo linalomgusa kila mmoja.
Alihitimisha hotuba yake kwa kutaja baadhi ya mambo yaliyosababisha Serikali kufanya marekebisho ya Sera hiyo. Mambo hayo ni pamoja na mabadiliko yanayotokea duniani kama mabadiliko ya tabianchi, uvumbuzi wa teknolojia mpya, kuibuka kwa wadau wapya wa maendeleo wenye nguvu na ushawishi na Watanzania wengi hawakuwepo wakati wa utungaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wwkiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana: Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Ikulu Zanzibar, Bw. Salehe Juma Mussa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Balozi Stephen Mbundi, Naibu Katiibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa, Mabalozi wa Tanzania Nje ya Nchi, Mabolozi Wastaafu akiwemo Balozi Amina Salum Ali, viongozi wa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia, Wakuu wa taasisi za Serikali na Sekta Binafsi, Wakuu wa Vyombo vya habari, wanazuoni na wananchi kwa ujumla.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Mhe. Salvador Valdés Mesa amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe 23 - 25 Januari, 2024.
Mara baada ya kuwasili nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mhe. Mesa alipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb.)
Akiwa nchini, Mhe. Mesa atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete na pia atatembelea taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Mhe. Mesa pia atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa za viuadudu ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Mahendra Siregar jijini Jakarta, kwa ajili ya kuangalia hatua za mwisho za maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itakayofanyika kuanzia tarehe 24-26 Januari, 2024 nchini humo.
Viongozi hao wamekubaliana kuwa maandalizi yote kwa ajili ya ziara hiyo yamekamilika na wako tayari kumpokea Mhe Rais tarehe 24 Januati atakapowasilo nchini Indonesia.
Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba amesema ziara hiyo ni muendelezo wa Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kayika kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Indonesia ambao mwaka huu unatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.
Ameongeza kuwa ziara hiyo pia inalenga kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia katika maeneo ya kımkakati ya biashara, uwekezaji, Afya, elimu, uchumi wa buluu na kilimo.
Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Siregar amesema Indonesia iko tayari kumpokea Mhe Rais Samia nchini mwao na kuahidi kuwa Indonesia inauthamini uhusiano wake na Tanzania na itaendela kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa na ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24-26 Januari 2024
TANZANIA, OMAN KUIMARISHA UTAMADUNI NA KUMBUKUMBU
Tanzania na Oman zimekubaliana kuimarisha sekta ya utalii kupitia utamaduni na kumbukumbu za mambo ya kale ili kuongeza utalii na kukuza uchumi wa mataifa hayo mawili kwa maslahi ya pande zote mbili.
Makubaliano hayo yameafikiwa na Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Urithi wa Mambo ya Kale na Utalii wa Oman, Mhe. Salim Mohammed Al Mahrouq kujadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Oman katika ukumbi wa Wizara hiyo.
Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadiliana na kukubaliana kuongeza fursa na ushirikiano katika nyanja za mafunzo na uzoefu kwa wataalam wa pande zote mbili. Adha, katika Utekelezaji wa mambo hayo, viongozi na wataalam wa Tanzania na Oman watakutana hivi karibuni kupanga mikakati ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano.
Mazungumzo hayo ni hatua ya utekelezaji wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Fatma Rajab ya kukuza ushirikiano wa kidiplomasia na Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

