WAZIRI MKUU AZINDUA KITUO ATAMIZI CHA UFUGAJI, KONGWA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 13, 2024 amezindua na kushuhudia makabidhiano ya Kituo Atamizi cha Ufugaji wa Kibiashara kwa Vijana kilichopo Kongwa mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya makabidhiano ya kituo hicho, ambacho kinathamani ya shilingi bilioni 1.63 ikijumuisha uwekezaji wa vifaa na mindombinu, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza uwekezaji utunzwe ili taifa liweze kunufaika kupitia uwezeshwaji wa vijana.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuwapatia vijana ujuzi kwa vitendo ikiwemo elimu ya ujenzi wa mabanda, ulishaji, matibabu na usimamizi wa mbuzi

lakini pia kutoa mafunzo ya biashara ili vijana waweze kuwa wajasiriamali na kuendeleza biashara ya unenepeshaji mbuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *