YANGA SC YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS SAMIA KATIKA KUTANGAZA UTALII

Na. Edmund Salaho/ Arusha

Rais wa Yanga SC Mhandisi.Hersi Said na Viongozi wa timu ya Soka ya Yanga watembelea Hifadhi ya Taifa Arusha leo Jumamosi tarehe 18/5/2024.

Ugeni huo umepokelewa na Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Yustina Kiwango pamoja na viongozi mbalimbali waandamizi wa Shirika.

Akizungumza baada ya kutembelea Hifadhi hiyo Rais wa Yanga Mhandisi Hersi alisema
“Sisi kama Wanachama,Viongozi na wapenzi wa Yanga tumekuja hapa kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais za kuitangaza Tanzania yetu lakini pia tutatumia fursa hizi kutangaza kazi za Mhe.Rais Nje ya Tanzania” alisema Mhandisi Hersi.

Aidha, Hersi aliongeza kuwa suala la Utalii sio suala la wageni kutoka nje pekee na kutoa rai kwa watanzania, wanachama na wapenzi wa Yanga kutembelea Hifadhi za Taifa.


“Sisi watanzania tuna nafasi kubwa ya kuchangia kwenye utalii wetu kupitia Utalii wa ndani lakini pia matangazo na kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais alizozifanya kupitia filamu ya “Royal tour” na sasa “Amaizing Tanzania”ambazo zimefungua mipaka kwa wageni kuja kufurahia vivutio vyetu”e

Akiukaribisha ugeni huo katika Hifadhi ya Taifa Arusha, Kamishna wa Msaidizi wa Uhifadhi, Yustina Kiwango alipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Klabu mbalimbali za michezo ambazo zimekuwa zikiiunga mkono adhma ya serikali ya Awamu ya sita katika kutangaza utalii wa nchi yetu na kutoa rai kwa wanachama kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kutangaza vivutio hivyo ndani na nje ya nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuvitembelea kwa wingi ili kuongeza pato la Taifa kupitia utalii wa ndani

Itakumbukwa Tarehe 20 Agosti, 2023 Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alishiriki kurekodi Filamu mpya ya kuitangaza Tanzania iitwayo “Amazing Tanzania” ambayo imezinduliwa rasmi Mei 15 mwaka huu jijini Beijing, China ikiwa imewashirikisha Marais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi ambapo kupitia filamu hizo tumeshuhudia idadi kubwa ya wageni wa nje ya nchi pamoja na mwamko mkubwa wa watalii wa ndani wanaokuja kuvitembelea vivutio vyetu na kuchangia katika pato la Taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *