Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Lusaka nchini Zambia, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ukarabati Mkubwa wa Reli ya TAZARA.

